Star Tv


Video kutoka katika vituo viwili vya televisheni vya Philadelphia Jumapili zilionesha vijana wakivunja magari kadhaa ya polisi na kuiba katika duka moja, lakini pia ripoti ya Uchunguzi ya West Philadelphia, imesema kuwa magari ya polisi yalichomwa moto.

Aidha, rais Donald Trump kupitia ujumbe ambao aliuandika twitter ulisema:Sheria na amri vifuatwe Philadelphia, SASA! Wanapora maduka.Walete wanajeshi wetu waingilie kati".

Tukio la Floyd limeibua ghadhabu miongoni mwa Wamarekani juu ya mauaji yanayotekelezwa na polisi dhidi ya watu weusi.

Hii inafuatia kesi maarufu ya mauaji ya Michael Brown mjini Ferguson, Eric Garner mjini New York na kesi nyingine zilizowasilishwa mahakamani na vuguvugu linalojulikana kama Black Lives Matters.

Kwa wengi ghadhabu ya kifo cha George Floyd pia inaonesha hasira juu ya kutokuwepo kwa usawa na kuwepo kwa ubaguzi katika masuala ya kijamii na kiuchumi, ambao haupo Minneapolis pekee.

Kikosi cha wanajeshi wa Ulinzi nchini Marekani- National Guard cha wanajeshi wa akiba kinachoshughulikia hali za dharura ndani ya nchi kimesema jana kuwa Wanajeshi wake 5,000 wamepelekwa katika majimbo 15 na Washington DC.

 

Latest News

TANZANIA, CHINA ZAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO.
10 Jul 2020 13:10 - Grace Melleor

Tanzania na China zimeahidi kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakuwa na maendeleo  [ ... ]

Breaking News: DKT HUSSEIN MWINYI APITISHWA KUWA MGOMBEA URAIS ZANZIBAR.
10 Jul 2020 10:45 - Grace Melleor

Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM umempitisha Dkt Hussein Mwinyi kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar baada ya kupata kura  [ ... ]

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA KUFANYIKA SIMIYU TENA.
08 Jul 2020 16:48 - Grace Melleor

Serikali imetangaza kuanzia tarehe 01 hadi 08 Agosti, 2020 kutafanyika maadhimisho ya sikukuu ya wakulima Nanenane ambap [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.