Star Tv

Waandamanaji nchini Marekani wamendelea kutanda nchini humo na kukabiliana na polisi katika miji mbalimbali kufuatia mauaji ya raia mweusi wa Marekani ambaye hakuwa na silaha aliyekufa mikononi mwa polisi huko Minneapolis.

Gavana wa Minnesota amesema kwamba kifo cha George Floyd aliyekuwa kizuizini kimeonesha mauaji ya kiholela, Huku New York, Atlanta na maeneo mengine yamekuwa yakishuhudia ghasia na Ikulu ya Marekani ikiwekewa katika hatua ya kusalia ndani kwa muda mfupi.

Aliyekuwa afisa wa polisi katika eneo la Minneapolis ameshtakiwa kwa mauaji kutokana na kifo hicho kwakua]wa tayari ameshakamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya mauaji baada ya kutokea kwa kifo cha mwanamume mweusi ambaye hakuwa na silaha aliyekuwa kizuizini.

Derek Chauvin, ambaye ni mzungu, alioneshwa kwenye video akipiga magoti juu ya shingo ya George Floyd mwenye umri wa miaka 46, Jumatatu. Yeye pamoja na maafisa wengine watatu wamekamatwa.

Maandamano ya siku kadhaa katika mji wa Minnesota yamesababisha uharibufu wa mali na kuchoma moto majumba ambayo pia yamesambaa katika maeneo mengine nchini Marekani.

Tukio hilo limesababisha hasira na ghadhabu nchini humo juu ya matukio mengine kama hayo ambapo polisi huwaua raia weusi wasiokuwa na hatia.

Mwendesha mashtaka Mike Freeman wa kaunti ya Hennepin alisema Bwana Chauvin alishtakiwa kwa makosa ya mauaji kiwango cha tatu huku kiwango cha pili kikiwa ni kuua bila kukusudia,
Aliongeza kuwa anatarajia kwamba wale maafisa wengine watatu pia nao watafunguliwa mashtaka lakini hakutoa maelezo zaidi.

Bwana Freeman alisema kuwa ofisi yake itaendesha kesi hii mara moja punde tu baada ya wao kupokea ushahidi.

Ripoti kamili ya madaktari bado haijatolewa lakini malalamishi yanasema kwamba upasuaji uliofanywa kama sehemu ya uchunguzi baada ya kifo cha Bwana Floyd, haukupata ushahidi wowote wa shinikizo la kubanwa kifua au kunyongwa.

Matokeo ya uchunguzi wa daktari yameonesha kwamba Bwana Floyd alikuwa na matatizo ya moyo na mchanganyiko wa yote hayo mawili, pengine vichocheo fulani katika mfumo wake na kukandamizwa na maafisa huenda kulichangia kifo chake.

Ripoti inasema kwamba Bwana Bwana Chauvin aliweka goti lake juu ya shingo ya Bwana Floyd na kumkandamiza kwa dakika 8 na sekunde 46 - karibia dakika tatu ambapo Bwana Floyd hakuamka tena.

 

Latest News

TANZANIA, CHINA ZAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO.
10 Jul 2020 13:10 - Grace Melleor

Tanzania na China zimeahidi kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakuwa na maendeleo  [ ... ]

Breaking News: DKT HUSSEIN MWINYI APITISHWA KUWA MGOMBEA URAIS ZANZIBAR.
10 Jul 2020 10:45 - Grace Melleor

Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM umempitisha Dkt Hussein Mwinyi kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar baada ya kupata kura  [ ... ]

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA KUFANYIKA SIMIYU TENA.
08 Jul 2020 16:48 - Grace Melleor

Serikali imetangaza kuanzia tarehe 01 hadi 08 Agosti, 2020 kutafanyika maadhimisho ya sikukuu ya wakulima Nanenane ambap [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.