Star Tv

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Cote d'Ivoire na kiongozi wa zamani wa waasi Guillaume Soro amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na kosa la wizi pamoja na utakatishaji wa fedha.

Guillaume Soro ambaye yuko ukimbizini nchini Ufaransa, hakuwepo wakati hukumu hiyo ilipotolewa na mahakama ya Abidjan Jumanne wiki hii.

Guillaume Soro na wanasheria wake wanasema hukumu hiyo ilitolewa na mahakama baada ya kushinikizwa ili kumzuia kuwania nyadhifa ya uongozi nchini humo.

Hivi karibuni Guillaume Soro alitangaza kuwania katika uchaguzi wa urais ujao nchini humo uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Soro anashtumiwa kwamba alitumia fedha za umma takribani Euro Milioni Saba kujinunulia makaazi ya kifahari jijni Abidjan mwaka 2007 alipokuwa Waziri Mkuu.

Hata hivyo washirika wake wa karibu ikiwa ni pamoja na ndugu zake, wabunge na wafuasi wake wanaendelea kuzuiliwa nchini Cote d'Ivoire baada ya kukamatwa tangu mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana.

Kulingana na wanasheria hao, kesi hii ni ya kisiasa na ilianza kwa sababu Guillaume Soro, mshirika wa zamani wa Alassane Ouattara, aliachana naye na kutangaza kuwania katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Latest News

FELICIEN KABUGA KUSHTAKIWA MAHAKAMA YA UN.
03 Jun 2020 17:11 - Grace Melleor

Mahakama nchini Ufaransa imeagiza Félicien Kabuga ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda kufikishwa [ ... ]

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI KESI YA SPIKA NDUGAI NA MWAMBE.
03 Jun 2020 14:49 - Grace Melleor

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wakili Paul Kaunda dhidi ya Spik [ ... ]

CHADEMA YAFUNGUA MILANGO KWA WANAOTAKA KUGOMBEA URAIS.
03 Jun 2020 14:33 - Grace Melleor

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefungua milango kwa wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea nafasi ya [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.