Star Tv

Rais wa Brazil Jair Bolsonaro anaweza kukabiliwa na mashtaka kufuatia kuanzishwa kwa uchunguzi baada ya mahakama ya juu nchini humo kuagiza uchunguzi kuhusu madai ya "kuingilia" katika kesi za mahakama, madai yalitolewa na waziri wake wa zamani wa Sheria.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Brazil Celso de Mello amewapa polisi muda wa siku 60 kumuhoji Sergio Moro, Waziri wa zamani wa Sheria na bingwa wa kupambana na ufisadi ambaye alijiuzulu kwenye nafasi yake siku ya Ijumaa, kulingana na uamuzi ambao shirika la habari la AFP limepata kopi ya taarifa hiyo.

Uchunguzi kama huo unaweza kufungua njia kwa utaratibu wa kutimuliwa madarakani dhidi ya Jair Bolsonaro, au kwa mashtaka dhidi ya Sergio Moro kwa makosa ya ushahidi wa uwongo.

Waziri huyu wa zamani maarufu nchini Brazili, na pia maarufu kwa operesheni yake ya kupambana na ufisadi "Lava Jato" yaani (kuosha haraka), alikabidhi barua yake ya kujiuzulu siku ya Ijumaa baada ya mkuu wa polisi nchini humo kufukuzwa kazi na mpaka sas jeshi la polisi nchini humo liko chini ya mamlaka ya Wizara ya Sheria.

"Kupinduliwa kwa mkuu wa Polisi bila sababu halisi ni kuingilia kisiasa Wizara ya Sheria, uamuzi ambao unaangusha sifa yangu na ile ya serikali,Rais aliniambia kuwa anataka kumteua mtu ambaye ana mawasiliano naye kibinafsi, ambaye atakuwa akimwita ili kupata taarifa kuhusu uchunguzi,"alisema Sergio Moro wakati akifanya mkutano na waandishi wa habari.

Rais Bolsonaro kwa upande wake alithibitisha hadharani siku ya Ijumaa kwamba madai hayo hayana msingi wowote na kuongeza kuwa waziri wake wa zamani alikuwa akijihusisha na mambo yake binafsi, hasa kuwa na kiti katika Mahakama Kuu.

Kulingana na Jaji de Mello, makosa yanayodaiwa dhidi ya rais yanaonekana kuwa na "uhusiano wa karibu na majukumu ya Rais", ambayo yanaomba kwanza aondolewe kinga.

Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Brazili unaonyesha makosa saba ambayo Bwana Bolsonaro anaweza kuwa alifanya, ikiwa ni pamoja na kutumia madaraka vibaya na kuzuia shughuli ya mahakama.

Aidha, Baada ya kujiuzulu, Bw.Moro alionesha kwenye runinga mazungumzo yake na rais Bolsonaro kupitia WhatsApp ambapo rais huyo akimshinikiza amfute kazi mkuu wa Polisi.

 

Latest News

FELICIEN KABUGA KUSHTAKIWA MAHAKAMA YA UN.
03 Jun 2020 17:11 - Grace Melleor

Mahakama nchini Ufaransa imeagiza Félicien Kabuga ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda kufikishwa [ ... ]

MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI KESI YA SPIKA NDUGAI NA MWAMBE.
03 Jun 2020 14:49 - Grace Melleor

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wakili Paul Kaunda dhidi ya Spik [ ... ]

CHADEMA YAFUNGUA MILANGO KWA WANAOTAKA KUGOMBEA URAIS.
03 Jun 2020 14:33 - Grace Melleor

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefungua milango kwa wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea nafasi ya [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.