Star Tv

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan ametupilia mbali ombi la Waziri wake wa Mambo ya Ndani Süleyman Soylu kutaka kujiuzulu.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki Süleyman Soylu jana Jumapili alitangaza kujiuzulu wadhifa wake katika wizara hiyo  kutokana na msongamano katika baadhi ya miji ya Uturuki, hasa baada ya kutangazwa amri ya kutotoka nje ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona.

Pamoja na hayo asubuhi ya leo vyombo vya habari nchini humo vimetangaza kuwa, Rais Recep Tayyip Erdoğan amekataa Waziri huyo asijiuzulu na kumtaka aendelee kubakia katika nafasi hiyo.

Amri ya kutotoka nje nchini Uturuki ilitangazwa Ijumaa usiku na punde kabla ya kutekelezwa kwake kwa tangazo hilo wakazi wa baadhi ya miji ya nchi hiyo ukiwemo mji wa Istanbul, walitoka kwenda madukani kwa lengo la kununua vyakula na vinywaji vyakujikimu.

Inaelezwa kuwa kama ombi la Waziri Soylu la lutaka kujiouzulu  lingekubaliwa, basi angekuwa waziri wa pili kujiondoa katika serikali ya Erdoğan baada ya kutangazwa kuenea virusi vya Corona nchini Uturuki, Na wiki mbili zilizopita, Waziri wa Usafirishaji wa nchi hiyo alijiuzulu wadhifa wake.
Hadi Jumapili ya jana Aprili 12,2020 idadi ya vifo vinavyotokana na virusi vya Corona nchini Uturuki vilikuwa 1198.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.