Star Tv

Rais wa zamani wa Congo-Brazzaville, Jacques Joachim Yhombi Opango, ambaye alitawala nchi hiyo 1977 na 1979, amefariki dunia.

Kifo chake kiliripotiwa na familia yake Jumatatu Machi 30 nchini Ufaransa kutokana na ugonjwa wa COVID-19 akiwa na umri wa miaka 81.

Kwa mujibu wa familia yake wamesema afya ya rais huyo wa zamani wa Congo-Brazzaville ilikuwa imezorota hivi karibuni, na kumlazimu kuishi mbali na nchi yake, ambapo alienda nchini Ufaransa na pia alikuwa akiishi nchini Ufaransa na Congo-Brazzaville tangu kumalizika kwa muda wake wa kuishi ukimbizini mwaka 2007.

"Baba yangu, rais wa zamani Yhombi Opango, alifariki dunia Jumatatu mchana katika hospitali ya Neuilly-sur-Seine karibu na Paris, Alikuwa muathirika wa ugonjwa wa Corona, "mtoto wake Jean-Jacques Yhombi Opango aliliambia shirika la Habari la AFP kwa simu.

Baada ya ya mtoto wa rais huyo kutoa taarifa hiyo, televisheni ya Congo-Brazaville (, Télé-Congo) ilichukua  hatua ya kuithibitisha taarifa hiyo kupitia familia yake baadaye jioni na kufahamu kuwa ni kweli rais huyo amefariki dunia.

Jacques Joachim Yhombi Opango alizaliwa mwaka 1939 huko Cuvette, Kaskazini mwa Congo-Brazzaville. Yhombi Opango, ambaye alikuwa afisa wa zamani, alichukuwa madaraka mara tu baada ya mauaji ya kuhuzunisha ya Rais Marien Ngouabi (1968-1977).

                         Mwisho.

Latest News

WAKILI AKIITA KIFO CHA GEORGE FLOYD MAUAJI YALIYOPANGWA.
01 Jun 2020 06:32 - Grace Melleor


Video kutoka katika vituo viwili vya televisheni vya Philadelphia Jumapili zilionesha vijana wakivunja magari kadhaa ya  [ ... ]

MAANDAMANO YAENDELEA KUTANDA MAREKANI KUFUATIA KIFO CHA FLOYD.
30 May 2020 10:22 - Grace Melleor

Waandamanaji nchini Marekani wamendelea kutanda nchini humo na kukabiliana na polisi katika miji mbalimbali kufuatia mau [ ... ]

RAIS MAGUFULI AKABIDHI TAUSI 25 KWA MAMA MARIA NYERERE NA MARAIS WASTAAFU.
30 May 2020 09:49 - Grace Melleor

Rais Magufuli leo May 30,2020 Mkoani Dodoma amewakabidhi Marais Wastaafu wa Tanzania kila mmoja Tausi 25 wanaopatikana I [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.