Star Tv

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo amedai kuwa serikali za Urusi na China zinajiepusha kutoa taarifa sahihi za virusi vya  ugonjwa wa Corona.

Pompeo ameyasema hayo katika mahojiano ya kipindi cha redio cha 'Washington Watch' ambapo akikariri madai yake ya huko nyuma juu ya kucheleweshwa na China taarifa za ugonjwa huo wa virusi vya Corona, a,mbapo amesema kuwa hali hiyo inahatarisha maisha ya maelfu ya watu wengi duniani.


Kadhalika Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ameendelea kudai kuwa Iran na Urusi pia zinatoa taarifa zisizo sahihi kuhusu virusi vya Corona.


Madai hayo ya Pompeo ni kutokana na radiamali kuhusu tuhuma zilizoelekezwa kwa Washington kwamba jeshi la Marekani ndio lililozalisha na kusambaza virusi vya Corona ambavyo vimeikumba pia chi hiyo.


Waziri huyo amesema kuwa serikali ya Washington iko chini ya mashinikizo makali ya ndani yanayosababishwa na usimamizi mbaya wa idara za kukabiliana na Corona.


Aidha Waziri Pompeo amenukuliwa akiendelea kutoa vitishokwa China kwamba baadaye Marekani itachukua uamuzi muhimu kuhusu uhusiano baina ya nchi hizo mbili (China na Marekani) utakavyokuwa.

                                Mwisho.

Latest News

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA KUFANYIKA SIMIYU TENA.
08 Jul 2020 16:48 - Grace Melleor

Serikali imetangaza kuanzia tarehe 01 hadi 08 Agosti, 2020 kutafanyika maadhimisho ya sikukuu ya wakulima Nanenane ambap [ ... ]

“SIJAJA CCM KUTANGAZA NIA”- JOSHUA NASSARI.
08 Jul 2020 15:46 - Grace Melleor

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amejiunga [ ... ]

WHO YATOA ANGALIZO JIPYA, USAMBAZWAJI WA COVID-19.
08 Jul 2020 08:41 - Grace Melleor

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kwamba "janga la Corona linaongezeka kwa kasi" na kukiri kwamba "ushahidi unaonye [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.