Star Tv

Wataalamu Wairani wamefanikiwa kutengeneza kifaa maalumu cha kupima kirusi cha Corona ambapo kifaa hicho ni cha kwanza cha aina hiyo kuundwa nchini Iran.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars,  limesema kifaa hicho cha kupima kirusi cha Corona kimeundwa na wataalamu Wairani katika Wizara ya Ulinzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kifaa hicho kilichoundwa nchini Iran kina uwezo wa kubaini iwapo mwanadamu ana kirusi cha  Corona mwilini na hivyo kutoa mchango mkubwa katika kukabiliana na kirusi cha Corona ambacho pia kinajulikana kama COVID-19.

Tangu kuthibitishwa kwa visa vya kwanza Disemba 2019, homa ya COVID -19 ya kirusi cha Corona ilisambaa na kuwa dharura kuu ya kiafya duniani, na kuua mamia ya watu na kuambukiza maelefu ya wengine.

Homa hiyo iliyoripotiwa  kwa mara ya kwanza katika mji wa Wuhan mkoani Huabei mashariki mwa China na sasa mbali na kuenea katika mikoa 30 nchini humo, homa hiyo ya Corona imeenea katika zaidi ya nchi 30 zikiwemo Iran, Marekani, Uingereza, Australia, Italia, Thailand, Korea Kusini, Japan, Canada, Ufaransa, Umoja wa Falme za Kiarabu au Imarati.

Kwa mujibu wa takwimu, hadi sasa watu wasiopungua 79,000 wameambukizwa kirusi cha Corona duniani, wengi wao  wakiwa nchini China na miongoni mwao 18,000 wamepata nafuu na kuruhusiwa kuondoka hospitalini huku wengine 2, 400 wakipoteza maisha.

                                                                 Mwisho.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.