Star Tv

Mshirika wa muda mrefu wa Rais wa Marekani, Donald, Trump ajulikanaye kwa jina la Roger Stone amehukumiwa kifungo cha miezi 40 jela.

Stone amehukumiwa adhabu hiyo baada ya kupatikana na hatia ya kuwadanganya wachunguzi na kuzuia sheria kuchukua mkondo wake katika uchunguzi kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi wa urais nchini Marekani mwaka 2016.

Jaji Amy Berman Jackson wa mahakama ya Marekani, amesema udanganyifu uliofanywa na Stone unatishia demokrasia ya nchi hiyo.

Hukumu hiyo imetolewa baada ya mwanasheria mkuu wa Marekani, William Barr kupunguza hukumu yake iliyopendekezwa kwa Bwana Stone ya miaka saba gerezani.

Mawakili wa Stone wameomba mteja wao awe chini ya uangalizi wa mahakama badala ya kutumikia kifungo chake gerezani, kwa kuzingatia umri wake ambao ni miaka 67, afya yake na kwa kuwa hana historia ya uhalifu.

                                                                                  Mwisho

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.