Mwana anga kutoka shirika la anga la Marekani NASA Christina Koch mwenye umri wa miaka 41, amerejea salama duniani baada ya kufanikisha kuingia katika rekodi ya kuwa mwana anga wa kwanza wa kike kudumu kwa takribani miezi 11 katika eneo la anga ya kimataifa.
Christina alitua katika eneo la Kazakhstan baada ya kudumu angani kwa siku 328, akiwa pamoja na Luca Parmito wa shirika la anga la Ulaya na Alexander Skvortsov wa shirika lingine kama hilo la Urusi.
Picha kutoka katika eneo la tukio zilimuonesha Christina akiwa mwenye tabasamu wakati ameketi kwa utulivu akiwa chomboni, ambaye alianza safari yake mwezi machi 14, 2019.
Mwisho.