Star Tv

Mamlaka za China zimesema kuwa watu 106 wamepoteza maisha kutokana na virusi vya Corona na zaidi ya watu 4000 wameambukizwa, wakati huohuo nchi hiyo imeweka katazo la kusafiri ili kuzuia maambukizi zaidi.

Mlipuko wa ugonjwa huo umekuja wakati wa sherehe za mwaka mpya ambazo huwakutanisha mamilioni ya watu nchini humo wakisafiri kuwatembelea ndugu na marafiki ambapo  miji mikubwa kadhaa imesitisha huduma ya usafirishaji wa Umma nchini humo.

Sherehe za mwaka mpya zilisogezwa mbele kwa siku tatu mpaka siku ya Jumapili, ili kudhibiti kuenea kwa maambukizi.

Idadi ya walioambukizwa kimataifa imeongezeka kukiwa na taarifa za maambukizi mapya huko Singapore na Ujerumani Mji wa Wuhan, ambao unaelezwa kuwa chanzo cha maambukizi ya virusi.

Kwa upande wa Marekani, ambayo ina maambukizi ya watu kadhaa, imewataka raia wake kufikiria upya suala la kusafiri kwenda China na imeshauri kutosafiri kwenda Hubei.

Nchi nyingine  zimetahadharisha safari za kwenda China huku wengine wakipanga kuwasafirisha raia wao waliokwama mjini Wuhan.

Taarifa zinaeleza kuwa mpaka sasa hakuna vifo vilivyoripotiwa nje ya China.

Virusi hivyo vinaelewa kuwa  havijawahi kutokea kabla ya mwezi disemba mwaka 2019 na vikapewa jina la "novel coronavirus".

Virusi vya aina hii huwa kwa kawaida vinawaathiri wanyama lakini mara nyingine vinaweza kuwapata binadamu, kwa mfano mlipuko wa ugonjwa wa 'Sars' ambao uliuwa watu wengi China kama ambavyo imeelezwa na wataalamu wa afya.

                                                                                                         Mwisho.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.