Star Tv

Japan itakuwa mwenyeji wa mkutano wa maendeleo na viongozi wa Afrika wiki hii, ikitazamia kuimarisha uwepo wake barani humo na kutoa mapendekezo mbadala kwa uwekezaji wa China inayozidi kujiimarisha barani Afrika.

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema anataka duru hii ya mkutano wa kimataifa wa Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika, TICAD, kusaidia kuzindua mkakati wa Japan wenye athari barani humo. Na mkutano huo, unaofanyika karibu kila miaka mitano tangu 1993 nchini Japan au katika nchi ya Afrika, unakuja wakati kuna ongezeko la uwekezaji nchini China, ambayo ilitangaza kiasi cha dola bilioni 60 katika ufadhili wa maendeleo ya Afrika mwaka jana. Kiasi hicho ni mara ya mbili zaidi ya ahadi ya Japan wakati wa mkutano wa TICAD mwaka 2016. Lakini wachambuzi wamesema Japan haina uwezekano wa kuipiku ahadi ya China katika mkutano wa mwaka huu, unaoanza kesho Jumatano na kumalizika siku ya Ijumaa.

CHANZO: Idhaa ya Kiswahili ya DW

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.