Star Tv

Raia wa Ukraine wanapiga kura leo katika uchaguzi ambao unaweza kushuhudia msanii wa vichekesho ambaye hajawahi kushika wadhifa wowote wa kisiasa akichaguliwa kuwa rais.

Volodymyr Zelenskiy, anaongoza katika kura ya maoni iliyofanyika kabla ya uchaguzi wa leo ingawa inaonekana hatopata wingi wa kura kumuwezesha kushinda moja kwa moja katika duru ya kwanza. Wananchi wa Ukraine wataamua kutoka miongoni mwa wagombea 39 wa urais waliojitokeza katika nchi hiyo yenye watu milioni 42. Ukraine inakabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo rushwa iliyokithiri pamoja na vita vinavyoendelea na waasi walio mashariki mwa nchi hiyo wanaoungwa mkono na Urusi.Rais Petro Poroshenko ambaye anawania muhula wa pili madarakani ana nafasi ndogo ya kushinda baada ya kura ya maoni kuonesha anaungwa mkono na asilimia 13.7 pekee ya wapiga kura.

CHANZO: Idhaa ya Kiswahili DW

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.