Star Tv

Rais Donald Trump wa Marekani amekubali ombi la Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un la kutaka wakutane mapema ndani ya mwezi mei mwaka huu,,,,

Rais Donald Trump wa Marekani amekubali ombi la Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un la kutaka wakutane mapema ndani ya mwezi mei mwaka huu,na hivyo kuweka historia kufuatia kuwa kutokuwepo rais wa Marekani ambaye amewahi kuonana na kiongozi mkuu wa Korea kaskazini.

Hata hivyo mahala watakapokutana viongozi panasalia kuwa siri kwa sasa,na pia Marekani imesisitiza kuwa pamoja na kukubali ombi hilo la rais Kim Jong Un laini bado vikwazo vitasalia pale pale.

Tangazo hilo la kwamba rais Trump amekubali kukutana na Kim Jong Un,limetolewa na viongozi wa juu wa Korea Kusini uliofika mjini Washington kuwasilisha barua ya ombi hilo kutoka kwa Korea Kaskazini.

Kim pia amekubali kusitisha mpango wake wa nyuklia na majaribio yake makombora,msimamo ambao ni tofauti na aliokuwa nao rais huyo Kim Jong Un.

Hatua hii iliyofikiwa ya rais Kim Jong Un kulegeza msimamo ni matokeo ya mazungumzo mazito yaliyofanywa wiki chache zilizopita ujumbe wa Korea Kusini kukutana na kiongozi huyo.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.