Star Tv
Mhubiri raia wa Marekani Billy Graham, mmoja wa wahubiri waliopata umaarufu mkubwa duniani katika karne ya 20 amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 99. Graham alipata umaarufu mkubwa kama mhubiri wa kikiristo akihubiri innji sehemu mbali mbali za dunia kwenye mikutano mikubwa akianzia London mwaka 1954. Kwa zaidi ya miaka 60 inakadiriwa kuwa alikuwa amehubiria jumla ya watu milioni 210. Alianza kujitolea kuwa mkiristo akiwa na miaka 16 babada ya kumsikiliza mhubiri mmoja na kutakaswa kuwa mhubiri mwaka 1939. Graham ambaye alikuwa amefanya kaza kama afisa wa mauzo alikuja kuibuka kuwa muungaji mkono mkubwa wa ukiristo. Mwaka 1949 alipata umaarufu wakati alihubiri kwa wiki nane kwenye hema kubwa huko Los Angels. Wakati wa harakati za mashirika ya kupigania haki za binadamu, Graham aliibuka kwa mkasoaji mkubwa wa ubaguzi wa rangi kwenye jamii nchini Marekani.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.