Star Tv
Binadamu kwa kawaida huwa macho mchana na usiku hulala, ingawa siku hizi si ajabu kwa wengi kulala mchana na kufanya kazi usiku. Lakini je, umewahi kujiuliza mwanadamu anaweza kukaa muda gani bila kulala? Vijana wawili nchini Marekani walijaribu kupima hili. Ilikuwa ni mwishoni mwa mwaka wa 1963 na bendi ya Beach Boys ilikuwa ndiyo inavuma zaidi wakati huo. Marekani ilikuwa pia imeanza kujiingiza zaidi katika Vita vya Vietnam, na watoto wa shule za upili walikuwa wanajiandaa kwa likizo ya Krismasi pale vijana wawili walipoamua kufanya utafiti ambao ulilivutia taifa. Utafiti huu ulifikia kikomo mnamo 8 Januaru 1964. Randy Gardner wa miaka 17 alikuwa amefanikiwa kukaa macho bila kulala kwa siku 11 na dakika 25 mfululizo. Bruce McAllister, mmoja wa wanafunzi wa sekondari walioibuka na wazo hilo, anasema hatua hiyo ilitokana na haja ya kuunda mradi wa kuwasilisha katika maonesho ya sayansi. Baada ya kuunganisha ubunifu wao na 'utukutu' kiasi wa ujana, Bruce na rafiki yake Randy waliamua kujaribu kuvunja rekodi ya dunia ya kukaa muda mrefu bila kulala. Rekodi hiyo wakati huo ilikuwa inashikiwa na DJ mmoja kutoka Honolulu, Hawaii ambaye alikuwa amekaa saa 260 bila kulala (siku 10 na saa 20). "Mpango wa kwanza ulikuwa wa kuchunguza athari za kutolala kwenye uwezo wa kiajabu usioeleweka wa ubongo (ikiwa ni pamoja na nguvu za kiroho)," McAllister anasema. "Tuligundua kwamba hakukuwa na njia ya kupima hilo na kwa hivyo tuliamua kupima basi athari za ukosefu wa usingizi kwenye uwezo wa mtu kufahamu na kutambua mambo, katika kucheza mpira wa kikapu. Jambo lolote tu ambalo tungeweza."

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.