Star Tv
Picha ya kusisimua ya sokwe na mmoja wa waokoaji wake imeshinda tuzo la mpigapicha bora wa mwaka la Chaguo la Watu au 'People's Choice'.Picha hii iliyoshinda tuzo la mwaka ilichukuliwa na mpigapicha wa Canada, Jo-Anne McArthur ilionesha sokwe huyo mdogo, kutoka eneo la nyika Tambarale ambaye aliokolewa na kampuni ya Ape Action Africa kutoka kwa wawindaji haramu. Katika picha hii anaonekana kwenye mikono ya mchungaji wake, Appolinaire Ndohoudou, wakati alipokuwa akisafirishwa kutoka kwenye makazi madogo ya sokwe hadi kwenye makao salama ya msitu wa Cameroon, ambako kuna msitu mpana zaidi. "'Ninashukuru sana kwamba picha hii imewagusa watu na ninatumai inaweza kutufundisha sote kuwajali walau kidogo wanyama," anasema McArthur. "Hakuna kitendo chochote cha ukarimu kwao kinachokua kidogo sana" "'Mara kwa mara ninarekodi ukatili wanaopitia wanyama katika mikono yetu, lakini wakati mwingine ninashuhudia taarifa za uokozi, matumaini na ukombozi wao." Picha hii ilichaguliwa takriban mara 20,000 na mashabiki wa mazingira kutoka kwenye orodha ya picha 24 zilizochaguliwa na makavazi ya kihistoria ya mali asili, ambazo zilichaguliwa kati ya picha from takriban 50,000 zilizowashilishwa kwa ajili ya shindano la kuwania tuzo la picha bora ya mwaka 2017.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.