Star Tv
Maafisa wa polisi nchini India wamemkatama mwanamke mmoja aliyejifanya kuwa mwanamume na kuwadanganya wanawake wawili ili kulipwa mahari. Krishna Sen alikamatwa siku ya Jumatano katika jimbo la Kaskazini la Uttarakhand kwa kutaka kulipwa mahari kinyume na sheria nchini India. Maafisa wa polisi waliambia BBC kwamba iligunduliwa wakati wa mahojiano kwamba Krishna alikuwa mwanamke. Wanaamini bi Sen mwenye umri wa miaka 26 aliyejulikana kama 'sweety' amekuwa akijidai kuwa mwanamume tangu 2014 wakati alipooa kwa mara ya kwanza.Bi Sen inadaiwa aliachana na mke wake wa kwanza mara tu baada ya harusi na mke wake wa kwanza na kumuoa mwanamke mwengine mnamo mwezi Aprili 2017. Lakini mashemegi zake waliwasilisha malalamishi wakimshutumu kwa kumnyanyasa mwanao ili kulipwa mahari. Pia walidai kwamba alikuwa amewaomba takriban dola 13,297 ili kuanza biashara na kwamba hakurudisha fedha hizo. Kulipa na kukubali mahari ni utamaduni wa karne moja iliopita Kusini mwa India ambapo wazazi wa mke hulipa fedha, nguo na vito kwa familia ya mume. Ijapokuwa utamaduni huo ni kinyume na sheria nchini India tangu 1961, unaendelea. Maafisa wa polisi walisema kuwa bi Sen aliwaambia kwamba amekuwa akitaka kuwa mvulana na kuishi kama mume akiongozea haijulikani iwapo wazazi wa bi Sen walikuwa wanajua kile ambacho amekuwa akifanya. Wanawake wote aliowaoa hawakumshuku. Bi Sen hakuvua nguo mbele yao na kulingana na polisi hakushiriki nao katika tendo la ngono. Alikuwa na marafiki wa kiume, akitumia vyoo vya wanaume na kuzungumza kwa kutumia sauti tofauti , polisi wanasema. Pia alidaiwa kuvuta sigara, kunywa pombe na kuendesha pikipiki na marafikize wa kiume, ili kuondoa shauku yoyote. Akiwa amenyolewa kama mwanamume, kuvaa na kuwa na tabia za kiume Krishna alikuwa akiishi maisha ya kiume. Hakuna mtu aliyemshuku Krishina, afisa mwengine wa polisi alisema.

Latest News

Kumbukumbu ya miaka 20 ya Hayati Mwalimu Nyerere
14 Oct 2019 12:52 - Kisali Shombe

Kila tarehe 14/10 Tanzania inaazimisha kumbukumbu ya kifo cha hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mwa [ ... ]

Mgogoro machimbo ya Shilalo Mwanza: Serikali yasitisha uchimbaji wa Dhahabu
11 Oct 2019 10:14 - Grace Melleor

Serikali imesitisha kwa muda usiojulikana shughuli za uchimbaji wa Madini ya Dhahabu katika machimbo ya Shilalo wilayani [ ... ]

Kesi Ya Uhujumu Uchumi: Sethi Na Rugemalira Waandika Kuomba Msamaha
11 Oct 2019 09:46 - Grace Melleor

Hayo yamebainika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo imeeelezwa, Seth aliandika barua yake iliyopitia kwa Mkuu [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.