Mwanamke mmoja wa China aliandamana na begi lake kupitia mashine ya ukaguzi ya X -Ray. Wafanyikazi katika kituo cha reli cha Kusini mwa China walishangazwa kuona mwanamke huyo akitoka ndani ya mashine hiyo pamoja na begi lake. Video moja ya mtandaoni ilionyesha kisa hicho cha kushanganza kilifanyika siku ya Jumapili baada ya kuupanda ukanda wa kusukuma mizigo. Awali mwanamke huyo alitazama begi lake likiwekwa katika mshipi huo na kuondoka.Picha za mionzi ya X-Ray zilimuonyesha mwanamke huyo akiwa amepiga magoti nyuma ya begi lake huku akiwa amevaa viatu virefu. Haijabainika ni kwa nini mwanamke huyo hakutaka kuwa mbali na begi lake ,lakini raia wengi nchini China hubeba kiwango kikubwa cha fedha wakati wanapoelekea nyumbani kusherehekea mwaka mpya.

Latest News

Kiwanda cha Alizeti chakosa malighafi, Mara
17 Jul 2019 13:12 - Kisali Shombe

Halmashauri ya wilaya ya Serengeti mkoani Mara imetenga zaidi ya shilingi milioni ishirini na tano ili kuwapa wakulima  [ ... ]

Mtendaji awekwa ndani kwa kula fedha za vitambulisho.
16 Jul 2019 14:01 - Kisali Shombe

Mkuu  wa  wilaya  ya  Kalambo Julieth Binyura  amemweka ndani  kwa muda  wa  saa 24 mtendaji  wa  kijiji cha  [ ... ]

Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 5 kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na M...
16 Jul 2019 12:49 - Kisali Shombe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 5 kuanzia leo tarehe 16 Julai, 2019 k [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.