Star Tv

Zaidi ya vijana 1,000 wameshtakiwa na polisi Denmark kwa kusambaza picha na video za ngono.

Wameshitakiwa kwa kutumia mtandao wa jamii wa Facebook Messenger kusambaza vipande vya video vilivyoonesha vijana wawili wenye miaka 15 wakifanya mapenzi.

Polisi wamesema kwa sababu vijana hao walikuwa wenye umri chini ya miaka 18, mashtaka yawaweza ongezeka hadi kosa la kusambaza picha zisizo ma maadili ya watoto.

Kampuni ya Facebook iiliwataarifu mamlaka wa Marekani ambao wakawatoa taarifa kwa polisi Denmark.

Kama wakipatikana na hatia ya kusambaza picha zisizo na maadili kwa watoto, watawekwa kwenye orodha ya wadhalilishaji ya watoto kingono kwa miaka 10.

Vijana elfu moja na nne wanamashtaka nchi nzima ikiwa ni baada ya kusambaza picha na video kwa kutumia app hiyo ya kutuma ujumbe mwishoni wa mwaka jana.

Baadhi ya watuhumiwa wenye umri juu ya miaka 18 waliitwa katika vituo vya polisi kuhojiwa.

Watuhumiwa chini ya miaka 18 wapatikana kupitia wazazi wao.

Mkuu wa polisi wa Denmark amesema mashitaka hayo yanakuja kama onyo kwa vijana kuthubutu kutuma video za ngono.

Yeyote atakayepatwa na hatia na mashtaka hayo anaweza kupata kifungo cha siku 20.

Kumekuwa na wito kwa serikali ya Denmark kuchukua hatua zaidi kuzuia picha za ngono ili kulipa kisasi.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.