Star Tv

Papa Farancis ameanza ziara yake nchini Chile huku kukiwa na wasiwasi wa kutokea shambulizi,kufuatia tishio lililotolewa kupitia vipeperushi vilivyo tolewa katika shambulio la awali kabla ya kuanza kwa ziara hiyo.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Dunian alipokelewa kwa shangwe na zaidi katika uwanja wa Santiago mji mkuu wa nchi hiyo,ambapo waumini wa kanisa Katoliki,viongozi mbali mbali wakiongozwa na rais wa Chile Michelle Bachelet walikuwepo pia.

Taifa la Chile lina zaidi ya asilimia 60 ya raia wake ni wakristo kati yao asilimia 45 ni wakatoliki,huku taifa hilo likiwa la pili katika bara la Amerika ya kusini kwa kuwa na idadi ya watu wasio na dini.

Hata hivyo ziara hii ya Papa nchini Chile imetanguliwa na matukio ya kushambuliwa kwa mabomu makanisa matatu mji mkuu wa taifa hilo Santiago huku washambuliaji wakiacha vipeperushi kwamba shambulio linalofuata ni dhidi ya Papa,kutokana na matukio hayo rais Bachelet amesema hayo ni matukio ya kushtusha.

Hii ni ziara yake ya kwanza nchini Chile tangu kuchaguliwa kwake,ziara hiyo ikikumbana na upinzani mkubwa kufuatia kashfa udhalilishaji wa kingono dhidi ya watoto unaodaiwa kufanywa na baadhi ya makaaisisi wa kanisa hilo nchini Chile.

Papa Francis leo anatarajiwa kukutana na waathirika wa ukatili wa kijeshi uliofanywa na dikteta Augusto Pinochet,ambapo pia zaidi ya nusu milion wanatarajiwa kuwa katika mkuasanyiko katika maeneo ambayo Papa atayatembelea katika ziara yake.Papa Francis amewasili nchini Chile ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya wiki moja nchini humo pamoja nan chi ya Peru.Sherehe za kumkaribisha Papa zimefanyika uwanja wa ndege wa Santiago.

Latest News

Kumbukumbu ya miaka 20 ya Hayati Mwalimu Nyerere
14 Oct 2019 12:52 - Kisali Shombe

Kila tarehe 14/10 Tanzania inaazimisha kumbukumbu ya kifo cha hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mwa [ ... ]

Mgogoro machimbo ya Shilalo Mwanza: Serikali yasitisha uchimbaji wa Dhahabu
11 Oct 2019 10:14 - Grace Melleor

Serikali imesitisha kwa muda usiojulikana shughuli za uchimbaji wa Madini ya Dhahabu katika machimbo ya Shilalo wilayani [ ... ]

Kesi Ya Uhujumu Uchumi: Sethi Na Rugemalira Waandika Kuomba Msamaha
11 Oct 2019 09:46 - Grace Melleor

Hayo yamebainika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo imeeelezwa, Seth aliandika barua yake iliyopitia kwa Mkuu [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.