Star Tv

Mti wa kale ambao umekuwepo Ikulu ya Marekani kwa karibu miaka 200 utakatwa.

Mti huo unaofahamika kama "Jackson" magnolia ulipandwa na rais Andrew Jackson kama kumbukumbu kwa mke wake.

Umekuwa ukionekana kwa picha wakati wa sherehe nyingi huko White House na hata picha zake ziliwekwa kwenye noti za dola 20 kati ya mwaka 1928 na 1988.Lakini wataalamu wanasema kuwa mti huo umeharibiwa na kuwa hatari kwa usalama. Mke wa Trump Melania Trump ametaka sehemu kubwa ya mti huo kukatwa.

Msemaji wa White House Stephanie Grisham anasema Bi Trump alichukua hataua hiyo kwa sababu mti huo ulikuwa ni tisho kwa usalama wa wageni na waandishi wa habari ambao mara nyingi husimama mbele yake wakati helikopta ya rais inapaa.

Mti wa Magnolia ulipandwa kutoka ya mji wa magnoalia uliokuwa ukipendwa na Rachel Jackson katika shamba lao huko Tennessee.

Marais 39 wamehudumu mti huo ukiwa White House na pia ulikuwepo wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Marekani na vita vya kwanza na vya pili vya dunia.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.