Star Tv

Waziri wa uchukuzi nchini Israel anataka kuchimba reli ya chini kwa chini kwenye mji wa zamani wa Jerusalem karibu na Ukuta wa Magharibi na kupewa jina la Donald Trump.

Yisrael Katz alisema kuwa anataka kumpa hushima rais huyo wa Marekani kufuatia uamuzi wake wa kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Ukuta wa Magharibi ndilo eneo takakatifu zaidi ambapo wayahudi wanaruhusiwa kuomba.

Reli hiyo mpya ya chini kwa chini na kituo cha treni na sehemu ya mradi wa reli ya mwendo kasi kutoka Tel Aviv ambayo inatarajiwa kuzinduliwa mwaka ujao.

Ujenzi wa awali eneo lililo karibu na Ukuta wa Magharibi ambalo hujulikana kwa waislamu kama Haram al-Sharif na kwa wayahudi kama Temple Mount imezua maandamano kutoka kwa wapalestina.Israel inautaja mji wa Jerusalem kuwa mji wake mkuu huku wapalestina wakilitaja eneo la Jerusalem Mashariki lililotwaliwa na Israel wakati wa vita vya mwaka 1967 kama mji mkuu wa taifa lake la baadaye.

Latest News

Kumbukumbu ya miaka 20 ya Hayati Mwalimu Nyerere
14 Oct 2019 12:52 - Kisali Shombe

Kila tarehe 14/10 Tanzania inaazimisha kumbukumbu ya kifo cha hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mwa [ ... ]

Mgogoro machimbo ya Shilalo Mwanza: Serikali yasitisha uchimbaji wa Dhahabu
11 Oct 2019 10:14 - Grace Melleor

Serikali imesitisha kwa muda usiojulikana shughuli za uchimbaji wa Madini ya Dhahabu katika machimbo ya Shilalo wilayani [ ... ]

Kesi Ya Uhujumu Uchumi: Sethi Na Rugemalira Waandika Kuomba Msamaha
11 Oct 2019 09:46 - Grace Melleor

Hayo yamebainika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo imeeelezwa, Seth aliandika barua yake iliyopitia kwa Mkuu [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.