Star Tv

Jose Maria Neves ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu kutoka 2001 hadi 2016 nchini Cape Verde ambaye ni kiongozi wa Upinzani amejitangaza kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.

Baada ya kupata chini ya asilimia 52 ya kura katika uchaguzi wa urais wa Jumapili nchini Cape Verde, mgombea wa upinzani Jose Maria Neves amejitangaza mshindi.

Matokeo ya awali ambayo yametangazwa kutoka asilimia 99.4 ya vituo vya kupiga kura pia zilionesha hasimu wake mkuu, Carlos Alberta Veiga, amepata 42% ya kura.

 

Bwana Neves, 61, aliwahi kuwa Waziri Mkuu kuanzia 2001 hadi 2016 na alikuwa mgombea wa cha kikubwa cha siasa cha African Party for the Independence of Cabo Verde (PAICV) nchini Cape Verde.

Wakati wa kampeni alisema kuwa akichaguliwa, atashughulikia mgawanyiko unaoshuhudiwa nchini, kufufua uchumi na kusuluhisha mzozo wa afya ulisababishwa na janga la corona.

Katika hotuba yake ya kwanza rasmi baada ya uchaguzi, alisema atakuwa "rais wa raia wote wa Cape Verde" na aliambia BBC kwamba "amefurahishwa sana na ushindi wake".

Mshindi alihitajika kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa ili kuepuka duru ya pili ya uchaguzi, ambapo wagombea saba walishiriki uchaguzi huo wa urais.

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.