Star Tv

Umoja wa Afrika (AU) pamoja na Umoja wa Mataifa (UN) umelaani mapinduzi nchini Guinea na kulitaka jeshi kumuachilia Rais Alpha Conde mara moja.

Katika taarifa Rais wa AU Felix Tshisekedi na Rais wa tume ya AU Moussa Faki wameitisha mkutano wa dharura wa taasisi za umoja huo kuhusu usalama na amani ili kutathmini hali nchini Guinea na kuchukua hatua zenye maslahi mapana.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres ametuma ujumbe wa twitter akijibu kinachotokea Guinea, Amesema kwamba anafuatilia hali hiyo kwa karibu.

Aliongeza kuwa alilaani kuchukuliwa kwa serikali kwa nguvu ya bunduki na akataka kuachiliwa mara moja kwa Rais Alpha Conde.

Hatima ya Rais wa Guinea Alpha Condé haijulikani wazi baada ya video ambayo haijathibitishwa kumuonyesha mikononi mwa wanajeshi, ambao walisema wamefanya mapinduzi.

Walakini, waziri wa ulinzi amenukuliwa akisema jaribio la kuichukua serikali lilikuwa limeshindwa.

Hii inafuatia masaa mengi ya makabiliano ya risasi karibu na ikulu ya rais katika mji mkuu, Conakry.

Jeshi ambalo limedai kuchukua madaraka nchini humo limetangaza kwamba litafanya mkutano leo na mawaziri na wakuu wa taasisi zilizovunjwa jana mjini Conakry, na pia wametangaza amri ya kutotoka nje kuanzia saa mbili usiku .

Wakijiita Kamati ya Kitaifa ya upatanisho na maendeleo, wanalaumu ufisadi uliokithiri, usimamizi mbaya na umasikini nchini Guinea kwa uamuzi wao wa kufanya mapinduzi.

Wanasema katiba imevunjwa na kwamba kutakuwa na mashauriano ya kuunda mpya, inayowahusisha watu wote .

Aidha, Wamedai pia kwamba serikali imevunjwa na kwamba mipaka ya ardhi itafungwa kwa wiki moja.

Katika picha na video zilizowekwa katika mitandao ya kijamii, mtu ambaye anaonekana kuwa rais Alpha Condé, amevaa mavazi ya kawaida na shati iliyochapishwa maua anaonyeshwa akiwa amekasirika akiwa amezungukwa na wanaume walio na sare za jeshi.

Ubalozi wa Australia umewauliza raia wake kukaa mahali salama na kutazama vyombo vya habari vya ndani na taarifa kutoka kwa balozi.

Wakazi wa eneo hilo wameambia mashirika ya habari kuwa wanajeshi wamekuwa wakifanya doria mitaani na wamefunga daraja kuelekea mtaa ambao ikulu ya rais iko.

Rais Conde alichaguliwa kwa muhula wa tatu uliokumba na utata ambao ulisababisha ghasia mwaka jana .Mwanasiasa huyo mkongwe alichaguliwa mara ya kwanza kuwa rais mwaka wa 2010 katika uchaguzi wa kwanza ulioshuhudia makabidhiano ya mamlaka ya njia ya Amani.

#ChanzoBBCSwahili

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.