Star Tv

Kundi la Wanamgambo wa Taliban limewazuia Wamarekani wanaoingia uwanja wa ndege wakati ndege ya Marekani inaondoka Afghanistan, ambapo bado kulikuwa na raia wa Marekani na Waafghani waliokuwa wakitarajia kuondoka na walikuwa wakijaribu kuingia kwenye uwanja wa ndege, maafisa wameeleza.

Katika mkutano wa waandishi wa habari awali, Jeneali McKenzie, Mkuu wa vikosi vya Marekani alithibitisha kuwa kuna Wamarekani 100-250 ambao wameshindwa kufika uwanja wa ndege au wameshindwa kuingia kwenye ndege.

Mwanajeshi wa zamani wa Marekani ambaye amesema kuwa alikuwa akisaidia kuratibu shughuli za uokoaji akiwa katika makazi yake Connectcut amesema Taliban waliwazuia wengi kupita. Alikuwa akiwasiliana na wengi, aliandika katika ukurasa wa twitter.

''Taliban walikuwa hawawezekani kuratibu nao mpaka mwisho. Walikataa kutoa ushirikiano nje ya milango ya kuingilia,''- Alisema.

Alex Plitsas, Mwanajeshi wa zamani amesema bado anawasiliana na Wamarekani wanaotaka kuondoka Afghanistan, lakini baadhi hawajajisajili kwenye mamlaka za Marekani, ''Hatuwezi kuwaokoa watu ambao hatujui kama wako huko,'' Alibainisha mwanajeshi huyo wa zamani.

#ChanzoBBCSwahili

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.