Star Tv

Msichana mmoja aliyejulikana kwa jina la Neha Paswan, mwenye umri wa miaka 17, anadaiwa kupigwa hadi kufa na watu wa familia yake katika jimbo la kaskazini la Uttar Pradesh kwasababu hawakupenda vile anavyovaa jeans.

Mama yake, Shakuntala Devi Paswan, aliiambia BBC Hindi kwamba msichana wake alikuwa amepigwa vibaya na fimbo na babu yake na wajomba zake baada ya kutokea kwa mabishano nyumbani juu ya nguo zake anazovaa katika kijiji cha Savreji Kharg wilayani Deoria, moja ya maeneo yenye maendeleo duni katika jimbo hilo.

"Alikuwa amefunga siku nzima kwendana na dini. Wakati wa jioni, akavaa suruali ya jeans na juu akawa na top au aina ya fulana kufanya ibada zake. Wakati babu na bibi yake walipinga mavazi yake, Neha alijibu kwamba jeans zilitengenezwa kwa ajili ya watu kuvaa"- Mama yake alisema.

Shakuntala Devi alisema wakati binti yake akiwa amelala baada ya kupoteza fahamu, wakwe zake waliita gari wakisema wanampeleka hospitalini.

"Hawakuniruhusu niandamane nao kwa hivyo niliwatahadharisha jamaa zangu ambao walikwenda hospitali ya wilaya wakimtafuta lakini hawakumpata"-Aliongeza Mama yake Neha.

Asubuhi iliyofuata, Shakuntala Devi alisema, walisikia kwamba mwili wa msichana mmoja umepatikana ukininginia kutoka kwenye daraja juu ya mto wa Gandak unaopita eneo hilo.

Walipokwenda kuchunguza, waligundua mwili huo ni wa binti Neha.

Polisi wamewasilisha kesi ya mauaji na uharibifu wa ushahidi dhidi ya watu 10, akiwemo babu na nyanya wa Neha, ami, shangazi, binamu na dereva wa magari, Ambapo washtakiwa bado hawajatoa tamko lolote kwa umma.

Afisa mwandamizi wa polisi Shriyash Tripathi aliambia BBC Hindi kwamba watu wanne, pamoja na babu na nyanya, mjomba na dereva wa magari, wamekamatwa na walikuwa wanahojiwa.

 

 

Latest News

KENYA YAPIGA MARUFUKU FILAMU YA WAPENZI WA JINSIA MOJA.
23 Sep 2021 14:44 - Grace Melleor

Bodi ya Filamu Kenya inasema kuwa filamu kuhusu maisha ya wanandoa wa jinsia nchini Kenya imepigwa marufuku nchini humo. [ ... ]

SHIL. MIL. 700 ZATOLEWA KUKARABATI BARABARA KARAGWE.
23 Sep 2021 13:55 - Grace Melleor

Serikali imetoa Shilingi Milioni 700 kusaidia ukarabati wa barabara za vijijini katika jimbo la Karagwe mkoani Kagera il [ ... ]

BABA AKAMATWA KWA KUCHOMA 'MATITI' YA BINTI YAKE.
22 Sep 2021 13:32 - Grace Melleor

Polisi katika jimbo la Nigeria la Lagos wamemtia nguvuni mwanaume mmoja kwa madai ya kuyaondoa matiti ya binti yake mwen [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.