Star Tv

Polisi wa Papua New Guinea (PNG) wameingia katika kituo cha mahabusu cha wahamiaji kilichokuwa kinamilikiwa na Australian kwa azma ya kuwaondosha wanaoomba uhamiaji waliosalia, imethibitisha serikali ya Australia.

Mamia ya wanaume wamekataa kuondoka kwenye kituo hicho kilichopo katika kisiwa cha Manustangu kilipofungwa tarehe 31 Oktoba, wakielezea hofu ya usalama wao.

Alhamisi, wanaume waliokuwa katika kituo hicho walisema polisi wa PNG walikuwa wamewapatia saa moja wawe wameondoka.

Australia imesema kuwa operesheni hiyo inaendeshwa na Papua New Guine- PNG.Chini ya sera tata, Australia iliwashikilia watu wanaoomba uhamiaji wanaowasili kwa boti kwenye kambi katika visiwa cha Manus na Nauru, ambalo ni taifa dogo leneo la Pacific.Australia ilifunga kituo hicho cha kisiwa cha Manus baada ya mahakama ya PNG kuamua kuwa kilikuwa ni kinyume cha sheria, na kuwataka wanaoomba uhamiaji kuhamia kwenye vituo vingine vya wanaoomba uhamiaji vilivyopo kwenye maeneo mengine ya kisiwa hicho.

Mmoja wa wakimbizi hao, Abdul Aziz Adam, alisema kwua watu wapatao 420 wanaoomba uhamiaji walibakia kwenye kituo hicho Alhamis Thursday, na walikuwa watulivu.

Watu hao walikataa kuondoka kwasababu wanahofia kuwa wanaweza kushambuliwa na jamii za watu waishio kwenye kisiwa hicho.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yansema wahamiaji hao wamewahi kushambuliwa awali.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.