Star Tv


Takriban watu 50 wanadaiwa kufariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi cha udongo katika mgodi wa dhahabu karibu na eneo la Kamituga mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, shirika moja lisilo la kiserikali katika eneo hilo limesema.

"Wachimbaji kadhaa walikuwa kwenye kisima ambacho kilifunikwa na udongo na hakuna mtu aliyeweza kuokolewa. Idnadaiwa kuwa vijana hamsini ndio walikuwa katika shimo hilo la mgodi,"- Kiongozi wa shirika moja la wanawake, Emiliane Itongwa.

Mkasa kama huo hutokea mara nyingi katika nchi mbalimbali duniani, na watu wameekuwa wakipoteza maisha kutokana na hali hiyo.

Jamhuri ya Kidemekrasi ya Congo ni nchi tajiri kwa dhahabu, almasi na coltan lakini migodi mingi inadhibitiwa na makundi yenye silaha, Huku watu wa DRC ni miongoni mwa watu maskini zaidi barani Afrika ingawa nchi hiyo ni tajiri kwa rasilimali.

Mashariki mwa DRC kumekuwa na migogoro kwa karibu miaka 24 sasa, huku wote jeshi na makundi ya waasi yakituhumiwa kutumia mapigano kama kisingizio wakati vikichota utajiri wa madini katika eneo hilo.

Wachambuzi wanasema soko la kimataifa kwa madini ya Coltan ni mojawapo ya vyanzo vya mgogoro na kuwepo kwa wanamgambo nchini humo.

Mwezi Mei 2011 serikali ya DRC iliondoa kizuizi kwenye machimbo ya Mashariki, eneo lililoathiriwa zaidi na migogoro ya muda mrefu.

CHANZO:rfi swahili.

Latest News

ETHIOPIA YASEMA HAITISHWI NA TAMKO LA RAIS DONALD TRUMP.
24 Oct 2020 16:54 - Grace Melleor

Waziri mkuu wa Ethiopia amesema nchi yake "haitakubali vitisho vya aina yoyote" baada ya Rais Donald Trump kusema kuwa M [ ... ]

RAIS TSHISEKEDI ATANGAZA MASHAURIANO YA UMOJA KWA MUUNGANO TAWALA.
24 Oct 2020 06:41 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi, katika hotuba yake kwa taifa aliyoitoa siku ya Ijumaa wiki hi [ ... ]

SEKTA YA AFYA NCHINI YAPATA NEEMA KUTOKA USWISI.
23 Oct 2020 15:23 - Grace Melleor

Serikali imepokea msaada wa Faranga za Uswisi Milioni 15.75 sawa na shilingi Bilioni 39.59 kwa ajili ya kugharamia mradi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.