Star Tv

Aliyekuwa makamu wa rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ambaye alifutwa kazi siku ya Jumatatu amelitoroka taifa hilo kufuatia vitisho vya kifo , kulingana na washirika wake.

Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 93 amemshtumu aliyekuwa makamu wake kwa kupanga njama za kuchukua mamlaka kutoka kwake.

''Alienda katika kanisa moja na Apostolic kujua ni lini Mugabe atafariki. Lakini aliambia kwamba atafariki wa kwanza'' , Mugabe aliwaambia wafuasi wake siku ya Jumatano.Mke wa rais Grace Mugabe sasa ndio aliye kifua mbele kumrithi rais mumewe.

Bi Mugabe amekuwa akipigania kung'atuliwa kwa makamu huyo katika mkutano maalum wa chama tawala cha Zanu-PF mwezi Ujao.

Chama cha Zanu PF kilimfurusha Mnangagwa katika chama hicho siku ya Jumatano.Bwana Mugabe alimtaja naibu wake wa zamani kuwa miongoni mwa waliopanga njama na akaonya kuwa atawachukulia hatua maafisa wengine wa chama hicho walioshirikiana na Mnangagwa.

''Tulimjua kitambo bwana Mnangagwa .Lakini hatukutaka kuwalezea. Alidhani kwamba kwa kuwa mwandani wangu nitambeba na kumpatia urais. Lakini sikufariki, na sikujiuzulu'', aliwaambaia wafuasi wake katika makao makuu ya chama cha Zanu PF mjini Harare.

''Tunatumai tutakabiliana na wengine ambao pia walikuwa na njama kama hiyo'' , aliongezea.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.