Star Tv

Watu watano wameuawa baada ya washambuliaji kuvamia kanisa moja Afrika Kusini wakati malumbano yanaendelea juu ya uongozi wa kanisa hilo.

Polisi Afrika Kusini imesema kwamba wamewanusuru wanaume, wanawake na watoto waliokuwa wametekwa nyara viungani mwa mji wa Johannesburg Jumamosi asubuhi.

Pia polisi wamewakamata watu karibia 40 na kunasa silaha kadhaa.

Walioshuhudia kisa hicho wanasema kwamba wanaume waliovamia kanisa la International Pentecostal Holiness walikuwa sehemu ya kundi pinzani.

Inasemekana kwamba uongozi wa kanisa hilo ni suala ambalo limekuwa likizua vurugu tangu aliyekuwa kiongozi wa kanisa hilo alipoaga dunia 2016.

2018, polisi waliwahi kuitwa kwenye kanisa hilo kufuatia mashambulio ya risasi miongoni mwa waumini, kulingana na ripoti ya shirika la ILO, Afrika Kusini, Huku mwaka jana, fedha za kanisa hilo zilikuwa angalizo baada ya kutokea kwa madai kuwa takriban randi milioni 110 sawa na ($6.5m; £5.2m) hazijulikani zilipo, kulingana nagazeti la The Sowetan .

Kulingana na msemaji wa kikosi cha polisi cha taifa, Brigedia Vish Naidoo, kundi la lililoshambulia lilifahamisha kundi lililokuwa ndani ya kanisa kwamba wanakuja kutwaa udhibiti wa jengo la kanisa

Alisema watu wanne wamepigwa risasi na kuchomwa moto hadi kufa wakiwa ndani ya gari, huku mlinzi wa jengo hilo ambaye inasemekana alijibu shambulio, pia naye amekufa baada ya kupigwa risasi.

Bunduki tano za rashasha, bunduki 16 na bastola 13 pamoja na silaha zingine zimepatikana ndani ya kanisa na kuchukuliwa na maafisa wa polisi kama ushahidi.

Idara ya Polisi ya Afrika Kusini imesema miongoni mwa waliokamatwa ni maafisa wa polisi wa idara hiyo, maafisa wa kikosi cha jeshi la Ulinzi, maafisa polisi wa mji wa Johannesburg pamoja na maafisa wa idara ya huduma ya magereza.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.