Mpaka wa Tanzania na Zambia umefungwa leo kwa muda kutokana na amri aliyoitoa rais wa nchi hiyo Edgar Lungu.
Kufungwa kwa mpaka huo hakujaamriwa ni lini mwisho wake lakini imeelezwa kuwa unafungwa muda tu.
Aidha, uamuzi huo wa Zambia kufunga mpaka huo unachukuliwa kama ni hatua kwao za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.
Waziri wa Afya nchini humo Chitalu Chilufya alinukuliwa akisema kupanda kwa visa hivyo ni vinatoka kwa miongoni mwa wafanyabiashara wa ngono na madereva wa Malori kwemnye miji ya mipaka nchini humo.
ongezeko la visa vya ugonjwa huo kufikia 267 nchini humo, ambapo mpaka sasa kumeripotiwa vifo 7 na wagonjwa waliopona 11.