Star Tv

Biashara nyingi zilizofunguliwa wiki iliyopita zimefungwa tena tangu mwishoni mwa wiki hii iliyopita katika maeneo kadhaa nchini Algeria, kwa sababu ya kutofuata kanuni zilizowekwa.

Kanuni hizo ni zile za kuzuia maambukizi ya virusi vya corona ikiwemo kutokaribiana kwa umbali wa mita moja kwa mujibu wa wataalamu wa afya.


Tangu kuanza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani zaidi ya wakuu 15 wa majimbo kati ya 48 wamejikuta hatua walizochukuwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona hazitekelezwi na wafanyabiashara pamoja na raia walio kwenye majimbo yao.


Kutokana na kadhia hiyo mamlaka nchininhumo imetoa agizo la kufungwa kwa biashara zote hasa maduka ya nguo, maduka ya viatu, migahawa na maduka ya mikate, yanayotembelewa sana wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, pamoja na maduka ya manukato.


Zaidi ya vifo 460 vimerekodiwa nchini Algeria tangu kuripotiwa kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya Corona, Februari 25, kulingana na Kamati ya Kisayansi inayofuatilia jinsi ugonjwa huo unavyoendelea nchini humo.


Tangu kuanza kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani Aprili 24, vifo 56 na kesi mpya 1,467 vimetangazwa kutokea ndani ya taifa hilo.

Siku ya Ijumaa rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune alitishia kuongeza masharti ya raia kutotembea ikiwa hatua za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona zitapuuzwa.

Aliporuhusu maduka kufunguliwa tena wiki iliyopita, Waziri Mkuu Abdelaziz Djerad aliwataka raia wa Algeria waendelee kuwa uangalifu kwa kuheshimu kanuni za usafi, hatua za kutokaibiana kwenye mbali wa mita moja na kujilinda.

Tangu Aprili 24, mwaka huu mamlaka nchini Algeria ililegeza masharti ya watu kutotembea katika Wilaya tisa huku lengo la katazo hilo likiwa ni kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.