Star Tv

Waziri Mkuu wa Sudan, Abdullah Hamdok amenusurika kuuawa baada ya msafara wake kulengwa kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.

Televisheni ya taifa ya Sudan imetangaza kuwa Hamdok amepelekwa katika eneo salama ambapo Mkurugenzi katika ofisi ya Hamdok ajulikanaye kwa jina la Ali bakhit amethibitisha kuwa kiongozi huyo yuko salama na hakuna mtu au kundi lolote ambalo limedai kuhusika na jaribio hilo la mauaji.

Hamdok aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Sudan mwezi Agosti mwaka 2019, baada ya maandamano ya kudai demokrasia kulilazimisha jeshi kumuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo, Omar al-Bashir na kukabidhi uongozi wa serikali kwa raia.

Karibu mwaka mmoja baada ya Bashir kuondolewa madarakani, Sudan inakabiliwa na mzozo wa kiuchumi.

Aidha, kwa mujibu wa Shirika la Fedha Duniani, mfumuko wa bei umefika asilimia 60 na kiwango cha ukosefu wa ajira kwa mwaka 2019 kilikuwa asilimia 22.1.

                  Mwisho.

 

Latest News

“HII CORONA IMETUWEKA KATIKA HALI NGUMU”-RAIS KENYATTA.
01 Jun 2020 14:21 - Grace Melleor

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameelezea wasiwasi wake kuhusu ongezeko la idadi ya watu walioambukuzwa virusi vya corona k [ ... ]

WAKILI AKIITA KIFO CHA GEORGE FLOYD MAUAJI YALIYOPANGWA.
01 Jun 2020 06:32 - Grace Melleor


Video kutoka katika vituo viwili vya televisheni vya Philadelphia Jumapili zilionesha vijana wakivunja magari kadhaa ya  [ ... ]

MAANDAMANO YAENDELEA KUTANDA MAREKANI KUFUATIA KIFO CHA FLOYD.
30 May 2020 10:22 - Grace Melleor

Waandamanaji nchini Marekani wamendelea kutanda nchini humo na kukabiliana na polisi katika miji mbalimbali kufuatia mau [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.