Raia wa Misri wanapiga kura ya maoni leo inayolenga kumpa nguvu zaidi Rais Abdel Fattah al-Sisi.
Kura hiyo iliyopingwa na makundi ya haki za binaadamu, inatazamiwa kuridhia mabadiliko makubwa ya kikatiba ambayo yataongeza muhula wa al-Sisi madarakani hadi mwaka 2024. Mbali ya hilo, kura hiyo pia itampa al-Sisi, mwenye umri wa miaka 64, nafasi ya kuwania tena kwa miaka sita baadaye, madaraka zaidi juu ya mahakama, na nguvu kubwa kwa jeshi kushiriki siasa. Bunge tayari limeshapiga kura wiki hii na kuunga mkono mabadiliko hayo, ikiwa ni pamoja na kurefusha muhula wa urais kutoka miaka minne hadi sita.
CHANZO:Idhaa ya Kiswahili DW