Tume ya uchaguzi nchini Misri imetangaza leo kwamba kura ya maoni kuhusu mageuzi ya katiba ikiwemo uwezekano wa kumruhusu rais Abdel-Fatah al sisi kubakia madarakani mpaka mwaka 2030,itafanyika Aprili 20-22.

Tangazo la tume hiyo limekuja baada ya hapo jana bunge la Misri kuidhinisha mageuzi ya katiba ambayo yatamruhusu rais el-Sisi kuendelea kujiimarisha madarakani. Maafisa wa Misri wanajaribu kuzuia kuongezeka kwa malalamiko yanayotolewa katika mtandao yakipinga mageuzi hayo. Bunge lenye wajumbe 596 linalohodhiwa na wafuasi wa el-Sisi lilihitaji wingi wa thuluthi mbili tu ya kura kupitisha mageuzi 14 na kuingiza vipengee vingine vingi vipya.

CHANZO:Idhaa ya Kiswahili DW

Latest News

Mauaji ya kukata makoromeo, washtakiwa wahukumiwa. Bukoba
20 Jun 2019 08:21 - Kisali Shombe

MAUAJI YA KUKATA MAKOROMEO:Washtakiwa wahukumiwa kunyongwa hadi kufa Mahakama kuu kanda ya Bukoba  imewahukumu  kunyo [ ... ]

Kudorola kwa soko la Pamba.
19 Jun 2019 12:20 - Kisali Shombe

Madiwani halmashauri ya wilaya ya bariadi mkoani Simiyu wameilalamikia serikali kuhusu zao la pamba kukosa soko la uhaki [ ... ]

Adha ya maji, Kalambo
19 Jun 2019 11:23 - Kisali Shombe

Wananchi  katika   kjiji cha  Kisungamile  kata  ya  matai   wilayani  Kalambo  mkoani  Rukwa  wameiomba   [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.