Bunge la Algeria litamchagua Rais mpya wa mpito wiki ijayo. Kwa mujibu wa shirika la habari la serikali -APS- zoezi hilo litafanyikakutokana na rais mkongwe Abdelaziz Bouteflika kujiuzulu kufuatia maandamano ya umma dhidi yake.
Bouteflika iliukatisha utawala wake wa miaka 20 baada ya jeshi kuacha kumuunga mkono tena, kufuatia maandamano ya wiki sita na miito ya kutaka mageuzi ya kidemokrasia nchini Algeria. Mwenyekiti wa sasa wa baraza la juu la bunge Abdelkader Bensalah huenda akateuliwa kushikilia wadhifa huo. Lakini Bensalah, sawa na Waziri Mkuu Nouredine Bedoui na Tayeb Belaiz, mkuu wa Baraza la Katiba wanakabiliwa na shinikizo la kuondoka kutoka kwa waandamanaji ambao wanawatazama kama watu wa karibu na mfumo wa sasa.
CHANZO: Idhaa ya Kiswahili DW