Star Tv

Kikosi kimoja cha majeshi ya Nigeria kimefyatua risasi angani kupinga amri ya kwenda mstari wa mbele kukabiliana na wanamgombo wa Boko Haramu. Vyombo vya habari vya nchi hivyo vimeripoti kuwa askari walikataa kupanda ndege ambayo ilikuwa iwahamishe kutoka Maiduguri katika mji mkuu wa jimbo la Borno kwenda katika mji wa Marte karibu na nchi jirani ya Niger.

Hali hiyo hakutarajiwa lakini ndivyo ilivyotokea katika jeshi la Nigeria siku ya jumapili, ambapo wanajeshi wa kikosi kimoja walipoonyesha kukataa kwenda mstari wa mbele kukabiliana na Boko haramu.

Mashuhuda wanasema mgomo huo uliendelea kwa takribani saa nane. Mwandishi wa BBC anasema kumekuwepo na hali ya kutotii amri miongoni mwa wanajeshi kwa miaka nane sasa. Kundi la Boko haramu limekuwa liikiendesha vitendo vya utekaji mauaji na hata vitendo vya ubakaji na ukatili.

Kumekuwa na maswali mengi kutoka miongoni mwa raia kufuatia kundi hilo kuendelea na vitendo vya kikatili huku majeshi Nigeria yakidai yanalidhibiti.

Kwa hisani ya BBC

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.