Star Tv

Mahakama nchini Rwanda imemkuta na hatia ya ugaidi Paul Rusesabagina katika kesi inayodaiwa na wafuasi wake kuwa imechochewa kisiasa.

Waendesha mashtaka wa Rwanda wametaka Rusesabagina, shujaa ambaye simulizi yake ilihamasisha filamu iliyopewa jina ''Hotel Rwanda'' ahukumiwe kifungo cha maisha.

Mtu ambaye alioneshwa katika filamu ya ''Hotel Rwanda'' kama shujaa aliyeokoa maisha ya watu wengi wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda amepatikana na hatia ya ugaidi katika mahakama nchini Rwanda.

Paul Rusesabagina alipatikana na hatia ya kulifadhili kundi moja la waasi akiwa mafichoni ambalo liliwauawa raia katika shambulio la 2018.

Familia yake imedai kwamba alichukuliwa na kupelekwa nchini Rwanda kwa nguvu.

Pia inasema kwamba mpendwa wao hakushtakiwa na mahakama huru.

Safari ya Rusesabagina kutoka mtu aliyekuwa na sifa chungu nzima hadi kuwa adui wa serikali ilianza wakati alipokuwa akiikosoa sana serikali.

Latest News

UFARANSA YAZINDUA MAGARI YA UMEME HAPA NCHINI.
20 Oct 2021 15:31 - Grace Melleor

Waziri wa Biashara na uchumi nchini Ufaransa Franck Riester amezindua magari ya umeme yaliyoundwa na kampuni ya E-Motion [ ... ]

UHITAJI WA NYAMA WAONGEZEKA NCHINI.
20 Oct 2021 15:23 - Grace Melleor

Serikali imesema malalamiko yaliyojitokeza hivi karibuni ya kupanda kwa bei ya nyama nchini yanaashiria ukuaji wa sekta  [ ... ]

UGANDA YAZINDUA GARI LA KIVITA LILILOUNDWA NCHINI HUMO.
19 Oct 2021 18:03 - Grace Melleor

Jeshi la Uganda limezindua gari la kivita lililoundwa nchini humo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.