Maafisa nchini Eritrea wamewaachilia kwa dhamana wafungwa 36 ambao wamekuwa mahabusu kwasababu ya imani yao.
Vyanzo vya habari vimeiambia BBC kuwa 14 kati ya wafungwa hao wamekuwa mahabusu kwa miaka minne iliyopita katika kisiwa cha Dahilik. Wengine 20 waliokamatwa mwishoni mwa mwezi uliopita wameachiliwa kwa dhamana.
Wafungwa wote wanatoka katika madhehebu ya Kiinjilisti na Kipentekoste.
Mwaka 2002 Eritrea ilianzisha sheria ambayo inazuia makanisa yote isipokuwa makanisa ya Orthodox, Katoliki na Lutherani, Aidha Waislamu wa madhehebu ya Sunni wanatambuliwa rasmi.
Serikali ya Eritrea imekuwa ikiwaachilia huru watu waliofungwa kwasababu za kidini.
Mwezi Septemba mwaka 2020, serikali ya Eritrea aliwaachilia mahabusu zaidi ya 20 ambapo walikuwa wamefungwa kwa miaka.
Mwezi Disemba, maafisa pia waliwaachilia wafuasi 28 wa kikundi cha Mashahidi wa Jehovah baada ya kutumikia kifungo cha jela kwa muda mrefu.
Wakristo wengi, bado wamebakia magerezani na wengine wamekuwa wakikamatwa mara kwa mara, kulingana na wanaharakati wa uhudu wa dini.
Serikali ya Eritrea inawashutumu Wakristo wa madhebebu ya Kipentekoste na kiinjilisti kwa kutumiwa na serikali za kigeni.
Eritrea, ambalo ni taifa lenye usiri, na la kijeshi kwa hali ya juu, imekuwa ikitawaliwa na Afwerki tangu ilipopata uhuru wak kutoka kwa Ethiopia mwaka 1993, bila uchaguzi au bunge na muswada wa katiba uliopo haujawahi kutekezwa.
Chanzo:BBCSwahili