Star Tv

Tembo 170 watapigwa mnada nchini Namibia kwa kile kilichobainishwa kuwa ni adha ya kuongezeka kwa ukame huku kukishuhudiwa ongezeko kubwa la tembo nchini humo.

Hii sio mara ya kwanza Namibia inauza wanyama kwa mnada, ambapo msimu wa kiangazi inaelezwa kuwa kunatokea mgogoro kati ya wanyama na binadamu ambao ndio unaifanya Namibia kuuza tembo hao 170 kwa mnada.

“Kwasababu ya ukame na kuongezeka kwa idadi ya tembo, na mgogoro kati ya tembo na binadamu, kumetambulika haja ya kupunguza idadi ya wanyama hao”- kwa mujibu wa tangazo lililowekwa katika gazeti la New Era linalomilikiwa na serikali.

Tangazo hilo lililowekwa na wizara ya mazingira ni zabuni ya kutafuta kampuni inayofikia mahitaji yanayotakikana ikiwemo viwango vya kimataifa na kibali cha usafirishaji wa wanyama.

Mwaka jana, nchi hiyo iliidhinisha uuzaji wa karibu wanyama 1,000 ambao walikuwa katika hatari ya kufa kwasababu ya ukosefu wa chakula.

Aidha, wanyama waliokuwa wanauzwa ni pamoja na tembo, nyati, twiga na pala lengo likiwa ni kupatikana kwa dola milioni 1.1 kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira.

Latest News

BIDEN KUSAINI MAAGIZO 12 YA RAIS.
17 Jan 2021 07:08 - Grace Melleor

Rais mteule wa Marekani Joe Biden atatia saini maagizo 12 ya rais siku ya kuapishwa kwake kuwa rais wiki ijayo ili kushu [ ... ]

MUSEVENI AWAONYA WAFUASI WA UPINZANI KUTOZUA GHASIA.
17 Jan 2021 06:10 - Grace Melleor

Rais wa muda mrefu nchini Uganda Yoweri Museveni jana Jumamosi ameonya kuwa vikosi vya usalama vitatumia nguvu kuzima ju [ ... ]

WATU WAWILI WANUSURIKA KUAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI.
17 Jan 2021 05:42 - Grace Melleor

Watu wawili wakazi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara wamenusurika kuawa na wananchi wenye hasira kali kutoka kwa vijana  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.