Star Tv

Desemba 1, 1990, Idriss Déby alichukua hatamu ya uongozi wa nchi ya Chad kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa, Hissène Habré.

Ni miaka miaka 30 tangu Idriss Déby, achukue madaraka kabla ya kupewa cheo cha marshal mwanzoni mwa mwaka huu.

Miaka 30 iliyopita, Desemba 1, 1990, akiwa kiongozi wa kundi la wapiganaji la Wokovu wa Uzalendo, MPS, Idriss Déby aliuteka mji wa Ndjamena, mji mkuu wa Chad alioukimbia mtangulizi wake Hissène Habré ambaye vikosi vyake vilishindwa kuhimili mashambilizi ya vikosi vya MPS.

Desemba 4 Idriss Débyaliteuliwa kuwa rais wa Baraza la taifa, wakati Hissène Habré akikimbilia Senegal.

Miezi ishirini mapema, mnamo Aprili 1, 1989, Idriss Déby na washirika wake wachache ambao walitafautiana na kiongozi wao Hissène Habré walijaribu kufanya mapinduzi.

Watu hao walioshirikiana na Idriss Déby, ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani Mahamat Brahim Itno, na Hassan Djamouss, Amiri Jeshi Mkuu wa jeshi la Chad.

Lakini mpango wao wa mapinduzi ulitibuliwa, washirika wake watatu na askari kadhaa walijaribu kuondoka Chad kuelekea Sudan.

Kutoka Sudan, Kanali Idriss Déby alifanikiwa kushirikiana na makundi mbalimbali ya upinzani dhidi ya Hissène Habré na mnamo Machi 11, 1990 aliunda kundi la wapiganaji la MPS katika eneo la Bamina nchini Sudan.

Rais wa Chad Hissène Habré wakati huo alikataa kutii agizo la mwenzake wa Ufaransa François Mitterrand, ambaye aliomba katika hotuba yake katika mkutano wa Ufaransa na Afrika huko La Baule mnamo 1989 kwamba serikali madarakani barani Afrika zinatakiwa kuanzisha mfumo wa vyama vingi na demokrasia ikiwa zinataka kuendelea kuungwa mkono na Ufaransa.

Habré, ambaye aliamua kupinga mamlaka ya zamani ya kikoloni, alipingana na kauli hiyo kwa kuandaa uchaguzi wake kwa muhula wa miaka saba mwezi Desemba 1989.

Uchaguzi wa wabunge uliruhusu kuanzishwa kwa Bunge ambalo halikuridhishwa na mfumo wake wa kidemokrasia.

Kulingana na baadhi ya wachambuzi, nia ya rais wa Chad kutumia mafuta ya Chad kwa gharama zote akiungwa mkono na Marekani ambapo alikuwa mmoja wa washirika wakuu katika vita dhidi ya Muammar Gaddafi wa Libya, ni mpoja ya sababu ya kuanguka kwa utawala wake.

Latest News

BIDEN KUSAINI MAAGIZO 12 YA RAIS.
17 Jan 2021 07:08 - Grace Melleor

Rais mteule wa Marekani Joe Biden atatia saini maagizo 12 ya rais siku ya kuapishwa kwake kuwa rais wiki ijayo ili kushu [ ... ]

MUSEVENI AWAONYA WAFUASI WA UPINZANI KUTOZUA GHASIA.
17 Jan 2021 06:10 - Grace Melleor

Rais wa muda mrefu nchini Uganda Yoweri Museveni jana Jumamosi ameonya kuwa vikosi vya usalama vitatumia nguvu kuzima ju [ ... ]

WATU WAWILI WANUSURIKA KUAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI.
17 Jan 2021 05:42 - Grace Melleor

Watu wawili wakazi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara wamenusurika kuawa na wananchi wenye hasira kali kutoka kwa vijana  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.