Star Tv

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, limesema kuwa waandamanaji kadhaa wanaopinga ukatili unaotekelezwa na Polisi mjini Lagos nchini Nigeria wameuawa.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, shirika hilo la kimataifa la Amnesty International limefahamisha kuwa polisi walilazimika kutumia risasi za moto na mabomu yakutoa machozi kuwatawanya waandamanaji zaidi ya elfu moja waliokuwa wamekusanyika katika mji wa kibiashara wa Lagos, nchini Nigeria.

Shirika hilo linasema waandamanaji kadhaa walipoteza maisha na maelfu ya wengine walijeruhiwa kwa kupigwa risasi, kwa mujibu wa mashuhuda.

Maandamano zaidi yameshuhudiwa kote nchini Nigeria kupinga kikosi maalum cha polisi cha kukabiliana na wizi (SARS) kikilaumiwa kwa kuendesha vitendo vya kikatili nchini humo.

Latest News

RAIS WA CHAD, IDRISS DEBY ATIMIZA MIAKA 30 MADARAKANI.
01 Dec 2020 14:48 - Grace Melleor

Desemba 1, 1990, Idriss Déby alichukua hatamu ya uongozi wa nchi ya Chad kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa, H [ ... ]

“HATUONDOKI CHADEMA, TUNAKATA RUFAA”- Halima Mdee.
01 Dec 2020 13:01 - Grace Melleor

Wabunge 19 wa viti maalum waliovuliwa uanachama wa chama cha upinzani Chadema, wamesema wataendelea kuwa 'wanachama wa h [ ... ]

MTANZANIA ALIYETEKELEZA SHAMBULIZI CHUO CHA GARISSA AJINYONGA GEREZANI.
30 Nov 2020 10:05 - Grace Melleor

Mtanzania Rashid Charles Mberesero aliyehukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2019 baada ya kupatikana na hatia ya kushiriki [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.