Star Tv

Nchini DRC, walimu kutoka chama cha walimu cha SYECO na wale kutoka chama cha walimu wa kikatolika (SYNECAT) wameanza mgomo wao leo Jumatatu.

Walimu hao wameandamana kwa kudai maboresho katika mshahara yao, Huku wakishuku pia uwepo wa makumi ya maelfu ya walimu hewa kwenye orodha ya malipo.

Baada ya ahadi zilizotolewa hasa na rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi, hali haibadiliki.

Leo Jumatatu, kati ya walimu ambao wameitikia wito wa kugoma na wale ambao wamefanya kazi ya kawaida, madai yao yanafanana.

Walimu wanasema kwamba bado kuna matatizo mengi na mwaka wa masomo haungepaswa kuanza kwa sasa.

Hivi karibuni baadhi ya vyama vya walimu viliamua kusogeza mbele mwaka wa masomo hadi Oktoba 26.

Uamuzi ambao ulifutiliwa mbali na mamlaka ya Wizara ya Elimu.

Kwa miaka kadhaa, maelfu ya walimu wamekuwa wanafanya kazi katika shule za umma bila hata kusajiliwa na serikali na wengi wao walikuwa hawalipwi mishahara yao.

Ili kutarajia kupata ufadhili wa Benki ya Dunia ya dola milioni 200 mwishoni mwa mwaka huu, serikali inatarajia kuanza kuwalipa. Walimu 58,000 wanatarajia kupokea, kwa mara ya kwanza, mshahara wao mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.