Star Tv

Nchini Mali, Waziri wa zamani wa Ulinzi Bah N'Daw, ataapishwa leo Ijumaa jijini Bamako kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo kwa muda wa miezi 18 ijayo, baada ya kuteuliwa na viongozi wa jeshi mapema wiki hii.

Sherehe za kumwapisha Bah N'Daw, ambaye pia ni Kanali mstaafu wa jeshi, zitahudhuriwa na msuluhishi wa mzozo wa Mali kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), Goodluck Jonathan, rais wa zamani wa Nigeria ni miongoni mwa wageni wengine mashuhuri kutoka eneo hilo.

N'Daw, mwenye umri wa miaka 70, alionekana kwa mara ya kwanza hadharani siku ya Alhamisi, alipokutana na msuluhishi huyo wa ECOWAS wakati wa mazungumzo ya ana kwa ana.

Uteuzi wake ulitangazwa siku ya Jumatatu na Kanali Assmi Goita, ambaye amekuwa akiongoza nchi hiyo baada ya kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani Ibrahim Boubakar Keita, Huku Kanali Goita, naye atahudumu kama Makamu wa rais.

Baada ya sherehe za leo, serikali itakayoongozwa na Waziri Mkuu ambaye atakuwa raia inatarajiwa kutangazwa na baadaye kuundwa kwa Baraza la Mawaziri.

Wakuu wa nchi za ECOWAS wanatarajiwa kuiondolea Mali vikwazo vya kiuchumi baada ya sherehe za leo za kumuapisha Rais huyo wa mpito.

Latest News

ETHIOPIA YASEMA HAITISHWI NA TAMKO LA RAIS DONALD TRUMP.
24 Oct 2020 16:54 - Grace Melleor

Waziri mkuu wa Ethiopia amesema nchi yake "haitakubali vitisho vya aina yoyote" baada ya Rais Donald Trump kusema kuwa M [ ... ]

RAIS TSHISEKEDI ATANGAZA MASHAURIANO YA UMOJA KWA MUUNGANO TAWALA.
24 Oct 2020 06:41 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi, katika hotuba yake kwa taifa aliyoitoa siku ya Ijumaa wiki hi [ ... ]

SEKTA YA AFYA NCHINI YAPATA NEEMA KUTOKA USWISI.
23 Oct 2020 15:23 - Grace Melleor

Serikali imepokea msaada wa Faranga za Uswisi Milioni 15.75 sawa na shilingi Bilioni 39.59 kwa ajili ya kugharamia mradi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.