Mwanasiasa mkongwe wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye, ambaye amewahi kuwania urais mara nne, ametangaza kuwa hatawania tena wadhifa huo wakati wa Uchaguzi Mkuu mapema mwaka 2021.
Besigye amewaambia wafausi wa chama chake cha FDC kuwa baada ya kutafakari kwa kina, ameona kutia nafasi kwa mtu mwingine kushiriki kwenye Uchaguzi huo.
Wachambuzi wa siasa nchini humo wanasema uamuzi huu unatoa nafasi kwa mwanasiasa kijana Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, ambaye ameonekana kupata uungawaji mkono kutoka kwa vijana wengi hasa waishio mijini.
Mwaka 2019 Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Waine na Dkt Kizza Besigye waliahidi kushirikiana kukiondosha madarakani chama tawala, National Resistance Movement (NRM) kinachoongozwa na rais Yoweri Museveni.
Besigye ambaye aliwahi kuwa daktari wa maungo wa rais Museveni alimpinga Museveni mara nne katika uchaguzi tangu mwaka 2001 lakini hakuweza kupata nafasi ya kushinda katika chaguzi zote hizo.
Besigye husifiwa sana kutokana na moyo anaoonyesha anapotoa hotuba zake na wengi wamemsifu kwa kusimama na kupinga utawala wa Museveni.