Star Tv

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameelezea wasiwasi wake kuhusu ongezeko la idadi ya watu walioambukuzwa virusi vya corona katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Akiwahutubia Wakenya katika sherehe za kuadhimisha miaka 57 ya Madaraka, rais Kenyatta alisema nchi hiyo inastahili kujikakamua kufikia malengo yake licha ya changamoto zinazosababishwa na janga la corona.

"Hii corona imetuweka katika hali ngumu lakini waanzilishi wa taifa hili walituasa tuwe wakakamavu nyakati kama hizi." Alisema Kenyatta.

Hii ni mara ya kwanza sherehe hizo zinafanywa kwa njia tofauti kulingana na muongozo wa kudhibiti maambukizi ya corona.

Bwana Kenyatta aidha, ameahidi kutoa maelezo zaidi kuhusu hatua zitakazochukuliwa na serikali yeke kurejelea shughuli za kawaida.
Awali katika mahojiano na kituo cha televisheni cha NTV, alisema wataalamu wanakadiria kilele cha maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 kuwa kati ya mwezi Agosti na Septemba.

Kiongozi huyo pia amesema Wakenya wanajukumu la kibinafsi la kuhakikisha maambukizi ya corona yanakomeshwa.

Kenya imekuwa ikiripoti ongezeko la idadi ya watu wanaombukizwa corona kila siku. Wizara ya Afya hivi karibuni ilatangaza kuongeza juhudi za upimaji hasa katika maeneo maalum ambako kumeripotiwa mlipuko wa wa virusi.

Kufikia sasa Kenya imethibitisha kuwa na watu 1,962, walioambukizwa virus vya corona idadi hiyo ikijumuisha vifo 64.

Rais Kenyatta pia amesema idadi ya maambukizi iko chini kwa sababu Wakenya wanafuata muongozo wa kinga uliotolewa na Wizara ya Afya
Pia amewapongeza wahudumu wa afya nchini kwa kujitolea kupambana na jana la corona.

Aidha, amewahimiza Wakenya kujiepusha na ukosoaji wa taifa usiokuwa na msingi kwani hali hiyo inaleta mvutano unaorudisha nyuma hatua iliyopigwa na serikali.

 

Latest News

TANZANIA, CHINA ZAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO.
10 Jul 2020 13:10 - Grace Melleor

Tanzania na China zimeahidi kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakuwa na maendeleo  [ ... ]

Breaking News: DKT HUSSEIN MWINYI APITISHWA KUWA MGOMBEA URAIS ZANZIBAR.
10 Jul 2020 10:45 - Grace Melleor

Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM umempitisha Dkt Hussein Mwinyi kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar baada ya kupata kura  [ ... ]

MAONESHO YA NANENANE KITAIFA KUFANYIKA SIMIYU TENA.
08 Jul 2020 16:48 - Grace Melleor

Serikali imetangaza kuanzia tarehe 01 hadi 08 Agosti, 2020 kutafanyika maadhimisho ya sikukuu ya wakulima Nanenane ambap [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.