Rais Uhuru Kenyatta amepinga kufanyika kwa mazungumzo yoyote na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini Kenya uliosababishwa na uchaguzi mkuu uliokwisha.

Katika hotuba yake muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa marudio , Rais Kenyatta amesema kuwa mpinzani wake mkuu Raila Odinga atakwenda mahakamani kwa mara nyengine tena kupinga uchaguzi wake.

Kenyatta amewataka wapinzani wake wa Nasa kutumia njia zote za kisheria katika kupigania haki yao.

Wawacheni mwanzo watumie njia zote za kisheria zilizosalia wawacheni wafanye wanachotaka.

Hakuna mtu yeyote atakayewadhulumu haki yao ya kikatiba.

''Kuhusu ajenda yangu ya kusonga mbele nitazungumza baada ya makabiliano ya mahakamani yamekwisha'' , alisema Kenyatta katika makao makuu ya tume ya uchaguzi katika eneo la Bomas jijini Nairobi.

Rais Kenyatta pia alimshutumu Raila Odinga kwa kujiondoa katika uchaguzi huo.

''Licha ya kwamba mpinzani wangu mkuu alienda mahakamani akitaka uchaguzi wa urais kufutiliwa mbali na akakubaliwa, aliamua kutotilia maanani uamuzi wote kwa pamoja ambao uliagiza kufanyika kwa uchaguzi katika kipindi cha siku 60 uliosimamiwa na IEBC.Baadaye alikaataa kushiriki katika uchaguzi''.

Katika uchaguzi wa marudio Uhuru alijipatia kura 7,483,895 huku Raila Odinga akijipatia kura 73,228 hata baada ya kujiondoa katika uchaguzi huo.

Latest News

Mauaji ya kukata makoromeo, washtakiwa wahukumiwa. Bukoba
20 Jun 2019 08:21 - Kisali Shombe

MAUAJI YA KUKATA MAKOROMEO:Washtakiwa wahukumiwa kunyongwa hadi kufa Mahakama kuu kanda ya Bukoba  imewahukumu  kunyo [ ... ]

Kudorola kwa soko la Pamba.
19 Jun 2019 12:20 - Kisali Shombe

Madiwani halmashauri ya wilaya ya bariadi mkoani Simiyu wameilalamikia serikali kuhusu zao la pamba kukosa soko la uhaki [ ... ]

Adha ya maji, Kalambo
19 Jun 2019 11:23 - Kisali Shombe

Wananchi  katika   kjiji cha  Kisungamile  kata  ya  matai   wilayani  Kalambo  mkoani  Rukwa  wameiomba   [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.