Star Tv

Shirika la Umoja wa mataifa la maswala ya wakimbizi UNHCR nchini Uganda limepata wasiwasi wa fungu la fedha la fedha walilonalo la wakimbizi katika mwaka huu wa 2018.

Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Uganda, Joel Boutroue amesema kufikia sasa wana asilimia 9% tu ya fedha jumla wanazotaka katika bajeti yao ya dola milioni 450 walizopanga kutumia mwaka huu.

Huenda shughuli za shirika hilo zikakwama kutokana na ukosefu wa fedha kutoka jamii ya kimataifa.Hilo litaathiri pakubwa usaidizi kwa mamilioni ya wakimbizi waliopo Uganda baadhi kutoka Uganda na hivi karibuni wengine wanaoonekana kuwasili nchini kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Boutroue anasema kwamba kwa sasa wamepokea dola milioni 40 kutoka kwa wafadhili.

Na wanatarajia nyongeza ya fungu kutoka Geneva kwani wafadhili wanachagia mfuko wa UNHCR kuendeleza shughuli zao na baadaye inabidi warudishe fedha hizo.

Ofisa ya waziri mkuu nchini Uganda inayoshughulika na maswala ya wakimbizi, inaonyesha takwimu za wakimbizi milioni 1.3 kufikia mwisho wa mezi wa nane mwaka 2017.

Ikiwa Milioni moja ni kutoka Sudan kusini na wengine kutoka DRC, Burundi, Somalia na mataifa mengine.

Mwaka 2012 Shirila la UNICEF katika mradi wa mswala ya binadamu ilitowa ripoti yake kwamba idadi ya wakimbizi nchini Uganda inatarajiwa kuongezeka zaidi kutoka milion 1.4 kufikia milioni 1.8 mwishoni mwa mwezi wa December mwaka 2018.

Boutroue ameongeza kusema kuwa Uganda imepokea wakimbizi 100,000 tangu mwezi wa January mwaka huu tokea DRC na Sudani kusini, na hivyo ametowa wito kwa jami ya kimataifa kutowa msaada wa dharura la sivyo watashindwa.

'Kama hatutapata misaada zaidi tuko katika hali ya hatari, nikisema sisi ni wakimbizi na watu wote wanaohusika na katika swala hilo.

Maana kama hatutapa fungu jingine mipango yote itaharibika.

Hatutaweza kuwalisha, kuwapa elimu na vingine bila ya vitu hivyo tunaweza kufikia katika hali mbaya zaidi.Na sioni kwa sababu gani, kwani Uganda ndio mama wa wakimbizi kutoka na sera zake nzuri na Amesema Joel Boutroue.

Kila mkimbizi anyewasili nchini Uganda anapewa kipande cha aridhi futi 50 kwa 50, vifaa vya ujenzi na mgawo wa chakula, na pia wakimbizi wanaruhusiwa kufanya biashara kama ana uwezo wa kufanya biashara popote nchini akiwa na kitambulisho chake cha ukimbizi.

Kwa hisani ya BBC.

Latest News

ZANZIBAR YAFUNGUA MILANGO KWENYE UTALII.
06 Jun 2020 10:30 - Grace Melleor

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeruhusu kuanzia leo safari za ndege za kitalii kuwasili nchini baada ya mambukizi ya [ ... ]

UFARANSA YATANGAZA KIFO CHA KIONGOZI WA AL-QAEDA.
06 Jun 2020 08:27 - Grace Melleor

Waziri wa Jeshi wa Ufaransa Florence Parly ametangaza kifo cha kiongozi wa al-Qaeda katika ukanda wa Maghreb (Aqmi) Abde [ ... ]

MZOZO WA SERIKALI YA LIBYA NA HAFTARI WAENDELEA KUSHIKA KASI.
06 Jun 2020 07:20 - Grace Melleor

Serikali ya Libya yadai kuuteka mji muhimu kutoka kwa hasimu wake Khalifa Haftar.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.