Wanawake wanaoishi vijijini huko Jamhumuri ya Kidemokrasi ya Kongo, hawana haki ya urithi wa mali pamoja na ardhi iliyoachwa na wazazi wao au waume zao. Na hii inatokana na mila na desturi zao zinazomtambua mwanaume kama mrithi pekee wa Ardhi.

Wanaharakati wa haki za wanawake nchini humo wako katika jitihada za kuwaelimisha jamii kuhusiana na madhara ya mila hizo. Wanaweke wanaoishi vijijini katika jimbo la Congo central hawana haki ya urithi mali au ardhi ya wazazi au waume zao.

Mila ya jimbo hilo inapinga kabisa kumpa mke urathi. Alphonsine Ponga ni mwanaharakati wa kutetea haki za akina mama katika kijiji cha Mbaza Ngungu. Yeye pia alikuwa mwathirika wa utamaduni huu.

Ponga ameeleza kwamba sheria ya Congo haina ubaguzi katika suala la urithi. Lakini katika hali kawaida , ni mila ndo imeendelea kukithiri zaidi ya sharia ya nchi hasa katika maeneo ya vijijini.

 

Latest News

Mauaji ya kukata makoromeo, washtakiwa wahukumiwa. Bukoba
20 Jun 2019 08:21 - Kisali Shombe

MAUAJI YA KUKATA MAKOROMEO:Washtakiwa wahukumiwa kunyongwa hadi kufa Mahakama kuu kanda ya Bukoba  imewahukumu  kunyo [ ... ]

Kudorola kwa soko la Pamba.
19 Jun 2019 12:20 - Kisali Shombe

Madiwani halmashauri ya wilaya ya bariadi mkoani Simiyu wameilalamikia serikali kuhusu zao la pamba kukosa soko la uhaki [ ... ]

Adha ya maji, Kalambo
19 Jun 2019 11:23 - Kisali Shombe

Wananchi  katika   kjiji cha  Kisungamile  kata  ya  matai   wilayani  Kalambo  mkoani  Rukwa  wameiomba   [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.